Lacazette kuivaa Rennes

LONDON, England

STRAIKA Alexandre Lacazette leo atakuwamo katika mchezo wa Arsenal dhidi ya  Rennes, baada ya klabu hiyo kukata rufaa ya kufungiwa kucheza mechi hiyo ya Ligi ya Europa na ikakubaliwa na Shirikisho la Soka Ulaya, UEFA.

Lacazette alilimwa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko Aleksandar Filipovic katika mchezo ambao Arsenal waliambulia kipigo cha bao 1-0 wakiwa ugenini dhidi ya BATE hatua ya 32 bora.

Kwa kosa hilo staa huyo alifungiwa kucheza mechi tatu akianza na marudiano baina ya timu hizo mbili na kisha akaikosa nyingine ya kwanza ambayo Arsenal walichapwa 3-1 wakiwa ugenini dhidi ya Rennes hatua ya 16 bora na hivyo alitarajiwa kuikosa tena na ya leo.

Hata hivyo, UEFA ilithibitisha juzi kwamba adhabu hiyo imepunguzwa na kuwa ya mechi mbili na nyota huyo ameshaitumikia na hivyo yupo huru kucheza mechi hiyo ya leo dhidi ya Rennes, itakayopigwa katika Uwanja wa Emirates.

 Msimu huu nyota huyo wa timu ya Taifa ya Ufaransa, ameshakifungia kikosi hicho cha  Unai Emery, mabao 14 katika mashindano yote na amekuwa na uelewano mzuri na staa mwenzake, Pierre-Emerick Aubameyang.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*