Kipa Biashara United atamani kutimka

NA MWAMVITA MTANDA

KIPA wa kikosi cha Biashara United, Nurdin Balora raia wa Burkinafaso, ameelezea kuchoshwa na manyanyaso anayoyapata ndani ya timu hiyo, hivyo anaona ni bora arudi kwao kuangalia maisha mengine.

Akizungumza na BINGWA jana, Balora alisema hali ya maisha imekuwa ngumu kwake tofauti na alivyotegemea, kwani  halipwi fedha zake kwa wakati.

“Kutokana na kiwango changu sikupenda  kuchezea timu ndogo kama hii, nilikuja hapa kuitumikia timu kubwa ya Yanga lakini mipango haikwenda vizuri, hivyo Biashara wakaniomba niwasaidie, sasa cha kushangaza ninakuwa katika wakati mgumu na siifurahii kazi yangu.

“Naona bora nirudi kwetu nikatazame mambo mengine, ninajua nitapata timu hata ikiwa ya nchi nyingine, kikubwa  nifanikiwe kuliko kuendelea kubaki hapa,” alieleza Balora.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*