Kiba, Alaine kupamba tamasha la Melanin Phunk Australia

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MFALME wa Bongo Fleva, Ali Kiba na nyota wa muziki kutoka Jamaika, Alaine na Dj maarufu nchini Afrika Kusini, Prince Keybee, wanatarajia kupamba tamasha la Melanin Phunk, katika Uwanja wa Batman Royal Coburg.

Kabla ya kutumbuiza katika tamasha hilo jioni ya leo kwa mara ya kwanza toka aanze muziki, King Kiba, atatumbuiza nchini humo katika usiku wa East Meets South.

Tamasha la Melanin Phunk, hufanyika kila mwaka nchini humo chini ya kampuni ya Iamike Entertainment na kuhusisha burudani za muziki mchanganyiko, chakula, vinywaji, maonyesho ya mitindo ya mavazi na nywele pamoja na ucheshi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*