Kagera kuwapa wachezaji Simba, Yanga

ZAINAB IDDY

KOCHA wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, amesema kuwa yupo tayari kuwatoa wachezaji wote watakaohitajika na timu za Simba na Yanga ili aijenge timu upya.

Akizungumza na BINGWA, Mexime alisema hana shaka na ubora wa ufundishaji wake, hivyo hata kama wakiondoka wachezaji wote ana uwezo wa kuisuka upya timu yake.

“Ni kawaida kwa Simba na Yanga kuchukua wachezaji katika timu ambazo zimewafunga, kwani tayari ipo idadi kubwa inatajwa kwenda huko msimu ujao.

“Sina wasiwasi wala mashaka, mchezaji yeyote ambaye anamaliza mkataba wake na Kagera ruksa kutoa taarifa za kuondoka kwake, ili nianze mchakato wa kuijenga upya timu kwa ajili ya msimu ujao,” alisema na kuongeza:

 “Kutokana na jinsi wachezaji wangu walivyozisumbua Simba na Yanga, nina hakika msimu ujao asilimia zaidi ya 50 ya waliopo sasa sitakuwa nao.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*