Johari afunguka kuwapa nafasi chipukizi

NA JEREMIA ERNEST

MWIGIZAJI mkongwe nchini, Blandina Chagula ‘Johari’, amesema alilazimika kupumzika kwa muda ili kuwapa nafasi wasanii chipukizi kuonyesha uwezo wao na mwaka huu amejipanga kurejea tena kwa kishindo.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Johari, ambaye ni miongoni mwa wamiliki wa kampuni ya RJ inayozalisha filamu nchini, alisema kimya chake kilifanya wasanii wachanga kupata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, hivyo kuongeza idadi ya ajira.

 “Ni kweli sijafanya kazi muda mrefu niliamua kusimama ili kuwapa nafasi waigizaji wachanga wajulikane na wao wapate riziki,” alisema Johari.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*