Bodi ya filamu yabariki mpango wa Binti Filamu

NA JEREMIA ERNEST

KATIBU Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisso, ameipongeza taasisi ya Binti Filamu inayoundwa na waigizaji wa kike nchini kwa kufanikisha tamasha la Kataa Mihadarati lililofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Fisso alivipongeza vyombo vya habari kwa kutangaza tamasha hilo lililokuwa na lengo kuwafikia watu 500 lakini takwimu zinaonyesha Kataa Mihadarati liliwagusa watu wengi zaidi.

“Nianze kwa kuwashukuru wanahabari kwa kuwashika mkono Binti Filamu mpaka wametimiza malengo, wasanii hawapaswi kutumika kama makontena ya kusambaza dawa za kulevya, bali wanapaswa kupinga biashara na matumizi ya dawa hizo,” alisema Fisso.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*