Aunt Ezekiel akana kushindwa kuuza pombe

NA JEREMIA ERNEST

MWIGIZAJI nyota Bongo, Aunt Ezekiel, amesema hajashindwa kuendesha biashara yake ya kuuza pombe katika pub yake iliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, bali amepata sehemu nyingine.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Aunt alisema kufungwa kwa pub hiyo kumefanya baadhi ya watu waseme amefulia, jambo ambalo si la kweli.

 “Sijashindwa kuendesha ‘pub’ yangu, ila nimepata eneo ambalo ni zuri zaidi, pia ni kubwa, linaweza kubeba watu wengi kuliko nilipokuwa mwanzo,” alisema Aunt.

Aliongeza kuwa kwa sasa anaendelea kufanya ukarabati wa pub yake mpya na ikiwa tayari atawajuza mashabiki wake.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*