Simba kuweka historia ya kufungua tawi Simiyu

Na Mwandishi Wetu, Simiyu Zaidi ya mashabiki 200 wa timu ya Simba Sport Club Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wamekutana kwa lengo la kuanzisha tawi la Simba Mkoani hapo. Mashabiki hao wamekutana leo Jumamosi Machi 23 ,katika Ukumbi wa Silk ulipo mkoani hapo. Ikumbukwe kuwa Tangu kuanzishwa kwa Mkoa wa Simiyu mwaka 2012 hakujawai kuwa na tawi lolote la timu […]

Wachezaji wakongwe waipa mbinu Taifa Stars ya kuiua Uganda

Elizabeth Joachim, Dar es salaam. Wachezaji wa timu ya Taifa (Taifa Stars) wamehaswa kuwa na upendo, ushirikiano na kutokuwa na ubinafsi ili washinde mechi ya kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon dhidi ya timu ya taifa la Uganda (The Craners) itakayopigwa Jumapili Machi 24 Uwanja wa Taifa. Wito huo umetolewa na baadhi ya mchezaji wa zamani wa timu ya taifa akiwemo, […]

Paqueta apania kufanya kweli na jezi ya Neymar

RIO, Brazil STAA Lucas Paqueta, amesema kwamba yupo tayari kuchukua jukumu la kuvaa jezi namba 10 ambayo ni maarufu katika kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil, baada ya kutokuwapo Neymar, ambaye ni majeruhi. Kwa sasa Brazil bado inaendelea na maandalizi yake kwa ajili ya michuano ya 2019 Copa America, wakati baadaye leo itakapoivaa Panama kabla ya kuivaa Jamhuru ya […]

Hazard: Huyo Tielemans atakuwa balaa

BRUSSELS, Ubelgiji STRAIKA Eden Hazard, amempongeza mchezaji mwenzake katika kikosi cha timu ya Taifa ya Ubelgiji, Youri Tielemans, kwa bao alilopachika usiku wa kuamkia jana na kuifanya timu yao kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Urusi na kusema kwamba anavyotarajia kiungo huyo wa Leicester City, atakuja kuwa tishio katika siku zijazo.  Katika mchezo huo wa kufuzu fainali za […]

Rooney ampa ukocha Solskjaer Man Utd

NEW YORK, Marekani NAHODHA wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, ni kama amempa kibarua cha ukocha kocha wa muda wa klabu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer, baada ya kusema kwamba anavyofikiri ndiye pekee anayewania kupewa mikoba hiyo kwa muda wa kudumu. Tangu alipokabidhiwa timu hiyo kwa muda, baada ya kufukuzwa Jose Mourinho, Desemba mwaka jana, Solskjaer, ameweza kurejesha hali ya […]

Stars Taifa lipo nyuma yenu

ZAITUNI KIBWANA NA WINFRIDA MTOI TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo inashuka dimbani kucheza na Uganda ‘The Cranes’, katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019). Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na Watanzania wengi wapenda soka, utachezeshwa na mwamuzi Eric Canstane kutoka Gabon kuanzia saa 12:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, jijini […]

Yanga yaandaliwa tiketi ya CAF kibabe

NA HUSSEIN OMAR YANGA imeandaliwa mapokezi ‘bab kubwa’ itakapowasili jijini Mwanza kucheza mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Alliance FC ya huko, lengo likiwa ni kuhakikisha inashinda na hatimaye kuzidi kuisogelea tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao. Mshindi wa michuano ya ASFC, atashiriki kipute cha Kombe la Shirikisho Afrika, wakati bingwa […]

USIYEMPENDA KAJA

Ronaldo alimwa faini, ruksa kuivaa Ajax  ROMA, Italia USIYEMPENDA kaja, hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya straika, Cristiano Ronaldo, kuruhusiwa kuwamo katika mchezo wa robo fainali unaoikabili timu yake ya Juventus dhidi ya Ajax, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ronaldo alikuwa aikose mechi hiyo, baada ya kufunguliwa kesi na Shirikisho la Soka Ulaya, katika Kamati yake ya Nidhamu […]

SIMBA NOMA, YATIKISA TP MAZEMBE

ZITUNI KIBWANA NA HUSSEIN OMAR TP Mazembe ya DR Congo imekiri kuwa kupangwa na Simba katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, inaweza kuwa mwisho wa safari yao katika michuano hiyo iwapo hawatakuwa makini, wakikiri kuwa kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao kinachonolewa na Mbelgiji Patrick Aussems, kinatisha. Timu hizo zimepangwa kukutana katika hatua hiyo baada ya […]